Meneja wa Habari wa Yanga, Ally Kamwe akizungumza na waandishi wa habari mchezo wa robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika watakaocheza dhidi ya Mamelodi Sundowns Machi 30, 2024 amesema mchezo huo amekabidhiwa mchezaji Mudathir Yahya Abbas na kwamba mchezo huo utaitwa 'Muda Day'.

Amesema mchezo huo amekabidhiwa mchezaji huyo kutokana na kujitoa kwake katika kuipambania timu ili kupata matokeo.

Aidha, ameongeza kuwa kutokana na staili ya kushangilia ya mchezaji huyo ya kupiga simu ndio sababu ya kukabidhiwa mechi hiyo ya kwamba mashabiki wapigiane simu kwaajili ya kujaza Uwanja wa Mkapa siku ya mechi hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement