Mara baada ya michezo ya jana, Azam FC wakipata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania huku Simba SC wao wakiibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Geita Gold, wote wanapointi 63, Azam FC akiwa nafasi ya pili na Simba SC akiwa nafasi ya Tatu tofauti ikiwa ni idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Ligi hiyo inaendelea kutimua vumbi hii leo, Yanga SC wakiwa ugenini dhidi ya Dodoma Jiji FC katika Dimba la Jamhuri Mjini Dodoma, Kocha wa Yanga SC Miguel Gamondi sambamba na Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji Kassim Liyogope wamezungumzia juu ya maandalizi ya mchezo huo kwa ujumla.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement