Kikosi cha Simba kimeanza safari kuelekea Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Mashujaa utakaochezwa kesho Aprili 9, 2024.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika kuanzia saa 10: 00 jioni.

Katika mechi mbili za mwisho timu hizi kukutana matokeo yalikuwa hivi.

Machi 15, 2024 mchezo wa Ligi Kuu Bara, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yakifungwa na kiungo mshambuliaji Clatous Chama mchezo ulichezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Februari 03, 2024 mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1- 0, likifungwa na Saido Ntibanzokiza.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement