BAADA ya kushinda kwa penalti mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Converty City, rasmi sasa Manchester United itakutana na Man City kwenye fainali ya michuano hiyo.

Man United ilishinda mechi hiyo kwa penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika dakika 120.

Katika mabao hayo matatu, Scott McTominay ndio alikuwa wa kwanza kuifunga Man United dakika 23, kabla ya Harry Maguire kupiga la pili dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kisha Bruno Fernandez akafunga la tatu dakika ya 58.

Converty ikaanza kusawazisha ambapo dakika ya 71 ilipata bao kupitia kwa Ellis Simmis, kisha Callum O'Hare akapiga la pili dakika ya 79 kabla ya Haji Wright kusawazisha kwa penalti baada ya Aaron Wan Bissaka kuushika mpira ndani ya eneo la hatari.

Katika penalti nyota wa Man United, Casemiro ndio alienda kupiga ya kwanza na kukosa ingawa ubao ulibadilika baada ya mastaa wawili wa Converty, Callum O'Hare na Ben Sheaf kukosa penalti ya tatu na nne.

Man City na Man United zitakutana kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za michuano hii baada ya kukutana msimu uliopita ambapo Man United iliambulia kichapo cha 2-1.

Mchezo wa fainali unatarajiwa kupigwa Mei 25, katika dimba la Wembley ambapo Man United itakuwa inatazamia kuchukua taji lao la 13 la michuano hii wakati Man City ikiwa ni la saba.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement