Watu wengi walimzoea katika masuala ya mpira wa miguu akiwa kama mchezaji na baadae kocha, lakini staa wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, Zinedine Zidane ‘Zizzou’ sasa ameamua kubadili fani kwa kugeuka dereva wa magari ya mashindano.

Gwiji huyo wa soka wa Ufaransa, alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la kihistoria la mashindano ya magari la Le Mans, ambalo madereva hushindana kwa saa 24 bila ya kusimama.


Mchezo huu huko Ufaransa una historia na heshima ambapo bingwa hutazamwa kama vile ameshinda Kombe la Dunia au Ballon d’Or katika mpira wa miguu.

Zidane alipewa heshima na kazi ya kufungua mashindano hayo kwa kuipeperusha bendera kabla ya madereva 62 kuanza kazi ya kuchuana.

Lakini kabla ya kupeperusha bendera kuashiria ruhusa kwa madereva waanze kushindana, Zidane alipewa nafasi ya kuwa mtu wa kwanza kuendesha gari katika barabara hiyo ya mashindano.

Alipewa funguo za kuendesha gari aina ya Alpenglow Hy4 ya Alpine.

Alionekana akiwa amevalia suti nyeupe kama dereva wa mbio hizo, huku akiwa ameshikilia kofia kabla ya kwenda garini.

Kabla ya kuanza kwa mbio hizo, Zidane alisema: “Saa 24 za mashindano ya Le Mans hazilinganishwi na kitu chochote, ni mbio za kipekee kwa yeyote anayependa mchezo wa magari, ni fahari kubwa kwa Ufaransa, binafsi najisikia furaha na naona heshima kufungua mbio hizi.”

Gari aliyoipanda Zidane ina uwezo wa kukimbia kwa kasi ya kilomita 167 kwa saa.


Baada ya kustaafu soka mwaka 2006, Zidane alihudumu kama Kocha wa Real Madrid kati ya 2016-2018 kabla ya kurejea 2019 na kukaa nayo hadi mwaka 2021.

Katika kipindi chote hicho alishinda mataji mawili ya La Liga, matatu mfululizo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya mwaka 2015 na 2018, Uefa Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia ya mwaka 2016 na 2017

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement