MCHEZAJI WA ZAMANI WA LIVERPOOL ROBERTO FIRMINO PAMOJA NA MKE WAKE WAIGEUKIA DINI
Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Timu ya Taifa ya Brazil, Roberto Firmino amekuwa mchungaji wa kanisa la Kiinjilisti ambalo alianzisha huko Maceio, Brazil, pamoja na mkewe Larissa Pereira.
Kupitia taarifa yao kwenye mitandao ya kijamii, Firmino na Pereira walisema tangu walipookoka na kubatizwa Mwaka 2020 wanatamani pia na watu wengine wauone upendo wa kristo juu yao.
"Tangu kukutana kwa mara ya kwanza na Kristo, tamaa iliwaka mioyoni mwetu, tunataka watu wahisi upendo huu uliotufikia. Sasa tuna hamu na wajibu mwingine kuwa wachungaji kwa niaba ya Mungu.” --- Wamesema.