Mchezaji Michael William wa klabu ya Mbuni amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuwazunguka wachezaji wa klabu timu ya Mbeya Kwanza waliokuwa kwenye benchi jambo ambalo lilitafsriwa kama kitendo kinachoashiria imani zakishirikina.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 41:5(5.5) ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

Klabu ya Mbuni imetozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa wachezaji wake kuwamwagia maji yenye utelezi na harufu mbaya waamuzi na kamishna wa mchezo tajwa hapo juu.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:25 ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Kutokana na kukithiri kwa matukio ya kiuamuzi yaliyozua utata katika mchezo huo, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imewapeleka waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu kwenye Kamati ya Waamuzi kwaajili ya kufanyiwa tathmini ya kiwango chao cha kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu katika mchezo huo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement