Mara baada ya kutamatika kwa Ligi ya NBC Championship msimu wa 2023/24 ni rasmi sasa Mbeya Kwanza waliomaliza na Pointi 65 wakiwa nafasi ya Tatu watacheza mchezo wa matoano kwa maana ya Play Off na Biashara United waliomaliza nafasi ya nne wakiwa na Pointi 62 kutafuta nafasi ya kupanda Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara.

Kwa upande wa Stand United walioshika nafasi ya 11, Green worriors nafasi ya 12, Transit Camp nafasi ya 13 na Copco walioshika nafasi ya 14 watacheza mechi za mchujo kusaka nafasi ya kusalia katika Ligi ya NBC Championship huku Pan Africans FC na Ruvu Shooting wakiwa wameshuka Daraja.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement