Mshambulizi wa Ufaransa Kylian Mbappe amesema klabu yake mpya ya Real Madrid haitamruhusu kucheza kwenye michezo ya Olimpiki 2024 huko Paris msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliwela dhamira yake ya kucheza nje katika Michezo yake ya nyumbani, hakuchaguliwa katika kikosi cha muda cha Olimpiki cha Ufaransa mnamo Juni 03 kwa sababu Real ilisema mchezaji yeyote anayeshiriki Euro 2024 hangeweza kucheza Olimpiki.

"Msimamo wa klabu yangu ulikuwa wazi sana, hivyo kuanzia wakati huo na kuendelea, nadhani sitashiriki katika Michezo hiyo," alisema Mbappe, ambaye ni sehemu ya timu ya Ufaransa itakayoanza kampeni ya Euro 2024 dhidi ya Austria mjini Dusseldorf Jumatatu ya Juni 17.

"Hivyo ndivyo ilivyo, na ninaelewa hilo pia, ninajiunga na timu mpya mnamo Septemba, kwa hivyo sio njia bora ya kuanza safari na sasa nadhani nitaitakia timu hii ya Ufaransa kila la heri, nitatazama kila mchezo. Natumai wataleta medali ya dhahabu nyumbani, " Amesema Mbappe.

Mashindano ya kandanda ya wanaume ya Olimpiki yataanza Julai 24 ikiwa ni siku 10 baada ya fainali ya Euro 2024 na kumalizika Agosti 09 ikiwa ni zaidi ya wiki moja kabla ya msimu wa La Liga kuanza.

Mashindano ya kandanda ya Olimpiki yanashindaniwa na timu za chini ya miaka 23 lakini kila taifa linaweza kujumuisha wachezaji watatu waliozidi umri katika kikosi chao.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement