Kylian Mbappe alifunga hat-trick wakati Paris St-Germain ilipoilaza Montpellier na kupanda juu kwa pointi 12 kwenye Ligue 1.

Vitinha alifunga bao la kwanza kabla ya Mbappe kufunga bao lake la kwanza kutoka pembezoni mwa kona.

Arnaud Nordin aliwafungia wenyeji naye Teji Savanier akawasawazishia.

Bao lake mshambuliaji wa Ufaransa dakika ya 50 lilipaa juu ya lango na kuingia wavuni kutokana na shambulkio kali huku Lee Kang-in na Nuno Mendes pia wakicheka na lango la PSG.

Mbappe sasa ana mabao 24 ya ligi kwa msimu huu baada ya kufunga hat-trick yake ya tatu kwenye kampeni.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement