Mashabiki wa Simba juzi usiku walitwaa Tuzo ya Mashabiki Bora wa michuano mipya ya African Football League (AFL). Mechi mbili tu dhidi ya Al Ahly, zilitosha kuiaminisha Afrika kuwa mashabiki wa Simba ni bora zaidi kuliko wa nchi za Kiarabu. Waliwashinda wale wa Al Alhy, Petro de Luanda, Esparence, TP Mazembe,

Wydad AC, Enyimba na mabingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza, Mamelodi Sundowns.

Mamelodi ilitwaa ubingwa huo kwa kuichapa Wydad AC kwa mabao 2-0 katika fainali ya pili iliyopigwa juzi Afrika Kusini baada ya ile ya kwanza iliyochezwa Morocco kupoteza kwa mabao 2-1, hivyo kutwaa taji kwa jumla ya mabao 3-2.

Kabla ya mechi ya Novemba 24 ya Simba, mastaa wa zamani na makocha wameshauri kitu.

Nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Mohamed Hussein Mmachinga' alisema inahitaji kuweka sawa mambo matatu akiyataja kuwa ni utulivu, unmoja na mshikamano na kusahau yaliyopita. "Simba kinachowatesa ni kitu kidogo tu, mchezo dhidi ya Yanga kufungwa bao nyingi vile. Sasa wanatakiwa kuungana kuondoa makundi ndani ya timu na kuwa kitu kimoja, naamini wataweza kupambana na wanaanzia nyumbani. Kuhusu kikosi wanacho kizuri tu sema wawe na utulivu," alisema Mmachinga.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Fikiri Magoso alisema: "Simba ya Roberthino ilikuwa na matatizo makubwa, inafunga lakini inafungwa mabao ya ajabu na laini sana. Kwa wasiojua mpira walikuwa wanawalaumu mabeki lakini ukweli fomula ya huyo kocha haikueleweka."

Aliongeza kuwa hata utimamu wa miili wachezaji wanapaswa kuwa nao zaidi ya ule wa sasa, huku kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime akisema kitakachoigharimu ni kuweka kichwani yaliyopita. "Naona Simba ina wachezaji wazuri sema watulize vichwa na kuiangalia mechi kwa ukubwa wake," alisema.

Philpo Alando, nyota wa zamani wa Azam FC alisema, "Hakuna nafasi hata ya kumpata mchezaji mwingine hadi dirisha dogo ambalo nalo ni muda mfupi na hata mashabiki wanatakiwa kujua timu yoyote duniani inapitia wakati mgumu hivyo wanatakiwa kuwapa moyo."

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement