Mashujaa haijaonja ushindi tangu ilipoifunga Ihefu kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Septemba 16, jambo ambalo limemfanya kocha wa timu hiyo, Abdallah Mohamed 'Baresi' kukiri hali ni ngumu kwao, lakini hawana namna wanajiopanga kabla ya kuwakabili majirani zao wa Tabora United kesho mjini Kigoma.

Mashujaa juzi ilikumbana na kichapo cha tano mfululizo katika mechi sita ilizocheza tangu ilipoonja ushindi wa mwisho kwa kuchapwa mabao 3-2 na KMC mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kocha Baresi alisema mambo ni magumu na wapo kwenye hali ngumu, lakini wanaendelea kupambana, Bares alikiri kupitia wakati mgumu huku akifunguka kuwa anahitaji kubadilika kimbinu kwani tayari wapinzani wake wamemjua njia zake hivyo wanatumia madhaifu hayo.

"Tulianza vizuri tumeonyesha ushindani wa kutosha sasa tunapitia mambo magumu ambayo ni muda wa kurekebisha kabla ya kurudi tulikotoka tunarudi tumekaribiswa sasa ni wakati wa kupambana. Ligi duru hili ni mgumu kila timu inatengeneza mazingira ya kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo kwakuwa tumeshindwa kuwa na muendelezo tumekubali kurudi uwanja wa mazoezi kusawazisha makosa." alisema. Bares baada ya kipigo dhidi ya KMC wanarudi nyumbani kuwakaribisha Tabora United huku akiweka wazi kuwa mchezo huo utakuwa muhimu kwao kurudisha morali na ushindani endapo watapata matokeo ya ushindi.

Hata hivyo, Baresi ana kazi kubwa mbele ya Tabora iliyotoka kupata ushindi wa 2-1 mbele ya Mtibwa Sugar, mbali na timu hizo kufahamiana kwani msimu uliopita zote zilikuwa Ligi ya Championship kabla ya kupanda.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement