MASHINDANO YA SAMIA MOTOCROSS CHAMPIONSHIP KUANZA JULAI 13
Kelvin Gabriel maarufu kama FBI ni mkazi wa Arusha na miongoni mwa washiriki wa mashindano ya kimataifa ya Pikipiki ya Samia Motocross Championship yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili Julai 13 - 14, 2024.
Kutokana na maboresho makubwa ya uwanja wa Lakilaki Kisongo, utakaotumika kwaajili ya mashindano hayo, Kelvin anaamini kwamba mazingira ya sasa ya uwanja huo yanaongeza ushindani na kumuweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuibuka mshindi katika msimu huu wa kwanza wa mashindano ya Samia Motocross Championship.
Kulingana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ambaye ndiye muanzilishi na mratibu wa mashindano hayo, Mshindi wa kwanza atajipatia Milioni 10, wa pili milioni 7, na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha shilingi Milioni 5 za Kitanzania kando ya zawadi nyingine mbalimbali.