Mashabiki watatu wa Valencia wamehukumiwa kifungo cha miezi 8 kila mmoja kwa makosa ya vitendo vya ubaguzi dhidi ya Nyota wa Real Madrid Vinicius Jr.

Vitendo hivyo vilimlenga Mwanasoka huyo wa Brazil kwenye mechi ya La Liga katika Uwanja wa Mestalla mnamo Mei 2023.

Kupitia mtandao wa X, Vinicius ameandika " Mimi si muhanga wa ubaguzi bali ni mtesaji wa wabaguzi".

"Wabaguzi wote muwe na hofu sasa, muone aibu na mjifiche,bila ya hivyo tutapambana"

"Hukumu hii ambayo ni ya kwanza katika historia ya Uhispania sio yangu ni kwa watu weusi wote"

"Asante La Liga na Real Madrid kwa msaada wenu hadi kuifikia hukumu hii ya kihistoria".

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement