Msiba wa Mwanariadha Kelvin Kiptum (24) haombolezwi Kenya pekee bali hata Chicago, Marekani wameguswa na kifo cha Mshindi huyu wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za Wanaume ambaye amefariki Jumapili iliyopita kwa ajali ya gari Nchini Kenya.

Kituo cha Televisheni cha CBS NEWS cha Chicago, ni miongoni mwa Vyombo vya habari vya Marekani vilivyotangaza taarifa za kifo hicho huku Mkurugenzi Mtendaji wa Chicago Marathon Carey Pinkowski akisema dunia imempoteza Mwanamichezo bora.

Pinkowski amesema atamkumbuka Kiptum kwa mengi ikiwemo unyenyekevu wake na wepesi wake wa kufikika na ambaye amefariki wakati safari yake kimichezo ikiwa ndio kwanza inaanza “moyo wangu umeumia, hatutomsahau….. tutamkumbuka daima”

Kiptum alikua miongoni mwa Wanariadha wapya wa Kenya wanaokuja kwa kasi huku akitokea katika hali duni ambayo miaka minne iliyopita ilimfanya ashiriki riadha kwa kutumia viatu vya kuazima baada ya kukosa uwezo wa kununua viatu vyake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement