Manchester City imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Premier League baada ya kuifunga West Ham United magoli 3-1 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kubeba taji hilo mara 4 mfululizo. 

Ushindi huo umeifanya City kufikisha pointi 91, ikifuatiwa na Arsenal yenye alama 89 baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Everton katika michezo ya kukamilisha Msimu wa 2023/24. 

Timu ya Liverpool ambayo imemuaga kocha wake, Jürgen Klopp imemaliza ikiwa nafasi ya 3 kwa pointi 82, Aston Villa ni ya 4 kwa kuwa na pointi 68. 

Staa wa Man City, Erling Haaland ameibuka Mfungaji Bora kwa kufikisha magoli 27. Upande wa pili Timu zilizoshuka Daraja ni Sheffield United, Burnley na Luton Town. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement