Klabu ya Manchester City wamezindua hatua za kisheria dhidi ya Ligi Kuu ya Uingereza kuhusu sheria za kifedha kabla ya kusikilizwa kwa kesi yao ya mashtaka 115.                                                

Imeripotiwa kwamba City inajaribu kukomesha sheria za Ligi ya Premia za Associated Party Transaction (ATP) ambapo sheria hizo zinahusu mikataba ya kibiashara na udhamini na makampuni yanayomilikiwa au kuhusishwa na wamiliki wa klabu moja.

Kwa jinsi mambo yalivyo, sheria hizo zinaamuru kwamba shughuli kama hizo zinapaswa kutathminiwa kwa uhuru ili kuwa na thamani ya soko.

Mzozo huo wa kisheria utasuluhishwa wakati wa kusikilizwa kwa upatanishi kwa wiki mbili kuanzia Jumatatu Juni 10.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement