1. HILI NI TUKIO JIPYA NA LA THAMANI DUNIANI

"Ni tukio jipya duniani, Afrika na hata Tanzania. Ni tukio pekee lenye thamani zaidi ndani ya wiki hizi mbili barani Afrika. Hii ndio michuano mikubwa zaidi barani Afrika na inashirikisha watu bora pekee na watu bora Tanzania ni Simba SC."

"Halijaja kwa bahati mbaya, ni kwa juhudi ambayo Simba imeifanya. Wakati wanapanga timu za kushiriki waliangalia timu zenye thamani na ubora. Kwanini Simba Sports Club ni sababu ya ubora wetu. Kila Mtanzania aseme asanteni na hongera Simba SC."

"Hili sio jambo la kawaida na sio tu mchezo lakini ni ufunguzi wa michuano hii. Hili ni jambo kubwa zaidi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu Tanzania."

"Hii ni African Football League ya kwanza duniani, mwakani na miaka ijayo timu zitaongezeka zaidi ya nane hivyo thamani yake haitakuwa sawa na sasa. Ni aibu siku hiyo uwanja ukiwa haujaa. Sio siku ya mtu kukosa."- Ahmed Ally.

2. VIINGILIO RAFIKI DHIDI YA AL AHLY

"Viingilio tumepanga kwa kuangalia hali za watu wetu.

Platinum - Tsh. 200,000

VIP B- Tsh. 40,000

VIP C - Tsh. 30,000

Machungwa - Tsh. 10,000

Mzunguko - Tsh. 7,000.

Hatutakuwa na VIP A sababu jukwaa limechukuliwa na FIFA na CAF."

"Tiketi tayari zimeanza kuuzwa vituoni."

3. TUTAZUNGUKA DAR NZIMA KUFANYA HAMASA

"Tutazunguka Dar nzima kufanya hamasa. Tarehe 14 ndio tutazindua wiki ya Kispika (Wiki ya Hamasa), tutazindulia Coco Beach. Kutakuwa na matukio mbalimbali kama mechi za mashabiki na pia kutakuwa na watu wa kuuza tiketi, watu wa NMB na CRDB kwa ajili ya watu kupata namba za mashabiki lakini pia jezi zitauzwa pale."

"Hii ni wiki yetu, kama kuna mtu kinamkera aende hata Tanga. Hiyo tarehe 14 tutaanzia maandamano kutokea makao makuu ya klabu kwenda Coco Beach. Tunatarajia kufika Coco majira ya saa 4 asubuhi."

"Jumapili itakuwa mapumziko kidogo. Jumatatu tutakuwa na Paint the City, hiyo siku ni kubandika vipeperushi kila sehemu. Kwenye mstimu, kwenye geti, kwenye magari. Hakuna mtu ambaye hatajua kama Simba inacheza tarehe 20."- Ahmed Ally

"Jumanne tutaanzia Mbagala kupita na kispika na tutaishia Manzese. Siku ya Jumatano tutakuwa na mkutano na Jeshi la Polisi kuzungumzia hali ya usalama. Ni tukio kubwa barani Afrika hivyo ni lazima tujiimarishe kwa usalama."

"Siku ya mechi kutakuwa na mabadiliko hivyo tukubali kufata maelekezo ambayo yatatolewa."

"Alhamisi ya tarehe 19 itakuwa mkutano wa makocha wa Simba na Al Ahly kuzungumzia maandalizi."- Ahmed Ally


4. SIMBA IMECHANGIA UKARABATI UWANJA WA MKAPA

"Mechi itachezwa saa 12:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa ambao na Simba imechangia ukarabati wake hivyo wajue wakicheza kwenye uwanja ule wanacheza sehemu ambayo Simba imechangia ukarabati."

"Watu wa African Football League wamefurahia ilivyokuwa programu ya Simba Day hivyo kwa kiasi kikubwa inafanana na kuna maboresho wamefanya."

"Kesho Alhamisi kikosi kitaingia kambini baada ya kumnyoa Singida Fountain Gate. Kuhusu wachezaji walioitwa timu za taifa tunaendelea na mazungumzo na mashirikisho ili wachezaji waliotwa wawahi kurudi ili tujiandae kwa ubora zaidi."- Ahmed Ally

5. TUNAENDA KUCHEZA NA TIMU BORA ZAIDI BARANI AFRIKA

"Tutacheza na timu bora zaidi Afrika, Simba SC tunaitamani ile namba moja ya ubora walionao. Ili tufanikishe hilo lazima tushirikiane kama Wanasimba. Hata wao wanafahamu wana kazi ngumu."

"Simba SC kuifunga Al Ahly sio jambo gumu, tunachokwenda kufanya safari hii ni kumtoa kwenye mashindano. Tunafahamu ubora wake lakini tunakwenda kufa nao. Hakuna kinachoshindikana chini ya jua."

"Kuanzia leo hadi Ijumaa siku ya mechi, Wanasimba sehemu yoyote agenda zetu tunapokutana ni kujadili African Footbal League. Kama watu wanataka tuzungumzie ligi sisi tupo keleleni hakuna wa kujadiliana nae. Wa pili na wa chini ndio waongee."- Ahmed Ally

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement