Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Suleiman Serera leo Aprili 8, 2024 wamefanya ziara katika Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya kukagua maendeleo ya chuo hicho ikiwemo ujenzi wa hosteli mpya unaoendelea kwa gharama ya shilingi Bilioni 2.56 itakayokuwa na uwezo wa kuchukua Wanachuo 192.


Viongozi hao pia wamekagua eneo la ujenzi wa Akademia ya Taifa ya Michezo inayojengwa katika eneo la chuo hicho kwa gharama ya shilingi Bilioni 31.5 ambayo itakuwa Kituo Cha Umahiri wa Michezo ikihusisha miundombinu mbalimbali ya michezo ikiwemo ya kuogelea viwango vya Olimpiki, viwanja vya mpira wa miguu, netiboli na riadha.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement