Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akipokea Kifimbo cha Mfalme wa Uingereza kuelekea Mashindano ya Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Glasgow Uingereza mwaka 2026. Amesisitiza umuhimu wa taasisi na mashirikisho ya michezo kuibua, kukuza na kuwezesha vipaji hasa miongoni mwa vijana wanaobeba matumaini ya Taifa.



“Kuwasili kwa Kifimbo cha Mfalme wa Uingereza ambacho kinabeba ujumbe wa uhifadhi wa mazingira hususani udhibiti wa taka za plastiki baharini kunapaswa kuikumbusha jamii wito wa kuchukua hatua na kuwajibika katika kutunza mazingira, pia Kifimbo hichi kinatoa fursa ya kutafakari juu ya umuhimu wa maandalizi ya mapema, ya kina na yanayoratibiwa vema katika kuelekea katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2026 huko Glasgow, “ Amesema Makamu wa Rais Mhe: Philip Mpango.                                                            



@wizara_sanaatz @nsc_bmt @olympictanzania

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement