MAJERAHA YAMUWEKA DILUNGA NJE YA “PITCH” KWA MIEZI MITATU
Mara baada ya kupata majeraha aliyoyapata Kiungo wa JKT Tanzania, Hassan Dilunga katika mchezo wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa uliopigwa Oktoba 30 mwaka huu katika Dimba la Chamazi, jijini Dar es salaam, taarifa rasmi imewekwa wazi kuwa kiungo huyo anatarajia kurejea Uwanjani baada ya miezi mitatu.
Katika Taarifa ya Daktari iliyotolewa na Klabu ya JKT Tanzania imeeleza kuwa, Dilunga aliumia mguu wa kulia eneo la Enka na kusababisha kuvunjika kwa mfupa mdogo unaoitwa Fibula, ambao husaidia mfupa mkuu kufanya kazi.
Taarifa ya Klabu hiyo imeeleza kuwa, mara baada ya kugundulika na tatizo hilo, alifungwa P.O.P ndogo itakayodumu kwa muda wa wiki moja na baada ya hapo atafungwa P.O.P kubwa itakayoondolewa baada ya mwezi mmoja na baadaye ataanza mazoezi mepesi baada ya miezi miwili.
Ikumbukwe, hiyo sio mara ya kwanza kwa Dilunga kutokuonekana Uwanjani kutokana na majeraha, alishawahi kukubwa na hali hiyo alipokuwa akiitumikia Klabu ya Simba mara baada ya kupata tatizo kwenye mguu wake na kupelekea kufungwa P.O.P.