Majeraha Yalimuweka Nje Rekondo Kwa Muda Mrefu Zaidi
Mwaka 2000 klabu ya AC Milan ilifanikiwa kunasa saini ya mchezaji Fernando Redondo katika klabu ya Real Madrid.
Fernando Redondo alikua na majeraha ya goti aloyoyapata katika uwanja wa mazoezi na alishindwa kucheza kwa ubora kwa kipindi cha miaka 2.
Fernando Redondo aliamua kusitisha kupokea kiasi cha £2.74M ambacho kilikua ni mshahara wake ndani ya klabu hiyo ya AC Milan.
Redondo pia alirudisha nyumba pamoja na gari ambalo uongozi wa klabu hiyo ulimkabidhi atumie kwa wakati huo.