MAHAKAMA NCHINI ITALIA IMEAGIZA KLABU YA JUVENTUS KUMLIPA MCHEZAJI WAO WA ZAMANI CRISTIANO RONALDO EURO MILIONI 8.3
Klabu ya Juventus imeagizwa kumlipa Cristiano Ronaldo euro milioni 8.3 ambayo inadaiwa na mahakama ya Italia.
Ronaldo, 39, alikubali kutochukua mshahara wake wakati soka nchini Italia liliposimamishwa na janga la Covid-19 msimu wa 2020-21
Mreno huyo anadai klabu yake ya zamani zaidi ya euro milioni 17.
Mahakama ya Usuluhishi wa mizozo ya michezo ilisema klabu hiyo inapaswa kulipa kile ambacho mchezaji huyo angepokea baada ya kukatwa kodi na makato mengine.
Ronaldo alichezea Juventus nchini Italia kwa misimu mitatu kati ya 2018 na 2021, akiwasaidia kushinda mataji mawili ya Serie A.
Aliondoka kwa kipindi chake cha pili akiwa na Manchester United na baada ya miezi 16 Old Trafford alijiunga na klabu ya Saudi Al-Nassr.
Mshindi huyo mara tano wa taji la Ballon d'Or - aliyetunukiwa mchezaji bora wa dunia - aliorodheshwa na jarida la biashara la Marekani la Forbes kama mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi mwaka wa 2023, akipokea mapato ya euro milioni 109.