Mohammed El Shenawy, kumbukumbu zinaonyesha kuwa ni kati ya vitu ambavyo vinamsumbua.

Katika mchezo wa msimu uliopita dhidi ya Mamelodi aliruhusu mabao mawili kwa mashuti ya nje ya 18, lakini mchezo uliopita kwenye Uwanja wa Mkapa ambao Simba ilishinda bao 1-0 aliruhusu pia bao la aina hiyo, lilowekwa na Luis Misquissone ambaye leo amepania haswa na alifanya mazoezi spesho.

Hata hivyo, upande wa Tshabalala, Simba watatakiwa kupawekea mkakati maalum kwa kuwa ni eneo ambalo staa Pecy Tau amekuwa akipatumia zaidi, lakini akiwa mchezaji mwenye kasi zaidi kwenye timu hiyo na kama Anthony Modeste waliomsajili kutoka Borrusia Dortmund atakuwepo basi Simba watatakiwa kuhakikisha wanaweka eneo lao la ulinzi badala ya kwenda na mfumo waliouzoea.

Modeste Raia wa Ufaransa ni kati ya washambuliaji mahiri akiwa na uwezo wa kupiga mashuti makali ya nje ya eneo la 18 la timu pinzani.

Simba kwenye mchezo huu pamoja na kutafuta ushindi itakuwa sehemu ya kuonyesha ukubwa wao kama alivyosema kocha wa Ahly,

Marcel Koller: "Kila anayecheza nasi mechi yake inakuwa maarufu zaidi, tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huu kikamilifu na tunafahamu tunakutana na timu bora."

Kama ilivyo kwa Kapombe na Tshabalala, Ahly nao wanawatumia Ali Maaloul na Mohammed Hany kama mabeki wa pembeni, wanauwezo zaidi wa kutengeneza nafasi kuliko kufunga, jambo ambalo kama Simba wakilitumia eneo hili wanaweza kupata mabao.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement