Mara baada ya kufanikiwa kuongoza katika nafasi ya Ufalme wa Soka nchini Afrika Kusini kwa kunyakua taji la saba mfululizo la ligi baada kwa kuwalaza Kaizer Chiefs bao 5-1 uwanjani Soccer City mjini Johannesburg, Kocha wa Klabu ya Mamelodi Sundowns Rulani Mokwena ameweka wazi kuwa huenda wasipate kikosi kama chake tena kwa muda mrefu ndani ya nchi hiyo.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Soka ya Afrika (AFL), ambao walishuhudia matumaini yao ya pili ya kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Afrika yakizimika baada ya kuondolewa na Espérance wiki moja tu iliyopita waliweka tabasamu kwenye nyuso za mashabiki wao kwa ushindi huo mnono wanaoupata.

Wakiwa wamevuka rekodi iliyowekwa mnamo mwaka 2005 na Kaizer Chiefs walipocheza mechi 31 bila kufungwa, Sundowns sasa inataka kuwa klabu ya kwanza kukamilisha msimu wa Premier League bila kupoteza ambapo wamesaliwa na mechi sita ambapo watawakaribisha Royal AM na Cape Town City huku wakisafiri kuwafuata Golden Arrows, Stellenbosch na TS Galaxy.

Ushindi huo wa Alhamisi dhidi ya Chiefs unawafanya mabingwa hao wa zamani wa kufikisha mataji yao ya ligi hadi 17 kwa jumla, rekodi inayowafanya waendeleze uongozi wao wa kuwa klabu iliyobeba mataji mengi zaidi ya ligi nchini Afrika Kusini mbele ya wapinzani wao Chiefs na Orlando Pirates.

Wakati mbio za kuwania ubingwa wa ligi zikiwa zimekamilika huku wakiwa na michezo sita mkononi, Lucas Ribeiro Costa wa Mamelody Sundowns akiwa na mabao 11 kwenye ligi yupo kwenye kinyang’anyiro cha kumaliza kama mfungaji bora wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza huku mbio za kuwania kiatu cha dhahabu zikiwa ni kati yake na Iqraam Rayners mwenye mabao 14 akikipiga na Stellenbosch FC pamoja na Tshegofatso Mabasa wa Orlando Pirates mwenye mabao 13.

Mataji ya ndani ya Mamelody Sundowns:

1988, 1989/90, 1992/93, 1997/98, 1998/99, 1999/2000, 2005/06, 2006/07, 2013/14, 2015/16, 2017/18, 2017/18, 2017/18, 2017/18. 2020/21, 2021/22, 2022/23, 2023/24.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement