Vital’O chini ya Kocha Sahabo Pariris ambao ndio Mabingwa wa Ligi kuu ya Burundi Primus Premier League 2023/2024 ndio watakaoiwakilisha Burundi katika Mashindano ya klabu bingwa Afrika 2024/2025 TotalEnergies.

Timu ya Sahabo ilimaliza na pointi 72 kutokana na mechi 30 ilizocheza, huku Flambeau du Center iliyofanya vizuri ilishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 69.

Vital’O ambao mara ya mwisho walinyakua taji la Ligi Kuu ya Burundi Primus msimu wa 2015/2016 wameshinda taji hilo mara 21. Inter FC wakiwa wametwaa taji hilo mara 9, huku Bumamuru FC wakiweka rekodi mara moja pekee msimu wa 2022/2023.

Klabu hiyo pia itaiwakilisha Burundi katika mashindano ya Cecafa Kagame Cup ambayo yatafanyikia jijini Dar es salaam mwezi Julai 20 hadi Agosti 4,2024.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement