MFUNGAJI bora wa muda wote wa timu ya Taifa ya Panama, ambaye alisaidia kulipeleka Taifa hilo kwenye fainali za kombe la Dunia 2018 Luis Tejada, amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 41 baada ya kudondoka uwanjani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyombo vya habari ndani ya Panama imeeleza kuwa Tejada, ambaye ana mabao 43 na timu ya taifa ambayo yanamfanya kuwa mfungaji wa muda wote m nchini humo alifariki akiwa anacheza moja ya Ligi za kukuza vipaji zilizokwenye mpango wa Shirikisho. 

Hata hivyo taarifa ya Shirikisho la soka nchini humo FEPAFUT imesema Tejada aliyekuwa kwenye mpango kazi wa kukuza na kuendeleza soka la vijana atakumbukwa daima na familia nzima ya wanamichezo sio tu Panama bali dunia kote. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement