Kocha wa PSG Luis Enrique ameeleza kuwa hawana wasiwasi juu ya kusaka mabao mawili hii leo mbele ya Dortmund ili kufika kufika Fainali Ligi ya Mbaingwa Barani Ulaya.

Enrique ameeleza kuwa Lengo sio kucheza ili kushinda kwa mabao mawili bali wamejipanga kwaajili ya kushinda zaidi.

PSG wanatazamia kurudia ushujaa wao katika robo-fainali, walipofungwa 3-2 nyumbani na Barcelona katika mechi ya kwanza lakini wakafuzu kwa ushindi wa 4-1 katika mchezo wa marudiano -- licha ya kuruhusu bao la kwanza nchini Uhispania.

Kwa upande wake Kocha wa Borussia Dortmund Edin Terzic amekiri mchezo wa Nusu Fainali Mkondo wa Pili Ligi ya Mabingwa kwao ni mchezo muhimu na mkubwa zaidi katika maisha yake ya soka hadi sasa hivyo wanahitaji kupambana zaidi kwaajili ya kuhakikisha wanatimiza malengo ya kufuzu Fainali.

Nusu Fainali Mkondo wa Pili Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inapigwa hii leo kwa mchezo wa kwanza PSG dhidi ya Dortmund huku kesho Real Madrid akimkaribisha Bayern.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement