Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anatazamiwa kujiuzulu nafasi hiyo mwishoni mwa msimu huu, akisema "ameishiwa nguvu".

Klopp aliteuliwa Oktoba 2015 na mkataba wake ulipaswa kumalizika hadi 2026.

Alishinda Ligi ya Mabingwa mnamo 2019 kabla ya kuiongoza Liverpool kutwaa taji lao la kwanza la ligi baada ya miaka 30 mnamo 2019-20.

"Niliiambia klabu tayari mnamo Novemba," alisema Klopp, ambaye ametangaza uamuzi wake na timu yake ambayo ipo kilele cha Ligi ya Premia.

"Ninaweza kuelewa kuwa ni mshtuko kwa watu wengi wakati huu, unapoisikia kwa mara ya kwanza, lakini ni wazi naweza kuielezea - ​​au angalau kujaribu kuielezea.

"Ninapenda kila kitu kuhusu klabu hii, napenda kila kitu kuhusu jiji, napenda kila kitu kuhusu wafuasi wetu, napenda timu, napenda wafanyakazi. Ninapenda kila kitu. Lakini kwa kuwa bado ninachukua uamuzi huu inakuonyesha kwamba nina hakika ndiyo hatua ninayopaswa kuchukua.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement