Staa wa Argentina na Klabu ya Inter Miami, Lionel Messi ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA 2023 kwa Wanaume akimshinda Erling Haaland aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Messi na Haaland wamelingana pointi 48 katika Mfumo wa upigaji kura uliowahusisha Walimu na Manahodha wa Timu za Taifa pamoja na Waandishi wa Habari za Michezo lakini Messi ameshinda kwa kuwa wengi amepata pointi 107 za kuchaguliwa kuwa "Chaguo la Kwanza" dhidi ya 64 alizopata Haaland.

Pamoja na hivyo, kwa kuwa Messi ni nahodha wa Argentina naye kura yake aliipeleka kwa Haaland akimchagua kuwa Mchezaji Bora wa FIFA.

Tuzo nyingine, Ederson ameshinda Kipa Bora wakati kocha wake wa Manchester City, Pep Guardiola akitwaa Tuzo ya Kocha Bora.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement