Mzunguko wa 29 Michuano ya NBC Championship kuendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii kwa mechi nane ambazo utaendelea kuzishuhudia hapa hapa TV3.

Tma atakaribisha Pamba FC Uwanja wa Black Rhino jijini Arusha, Pan African dhidi ya Biashara United Uwanja wa Meja Generaji Isamuyo jijini Dar es salaam, Dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha litawakutanisha Mbuni FC dhidi ya Copco FC na Cosmopolitan dhidi ya Stand United dimba la Mabatini Mkoani Pwani.

Mechi nyingine ni Polisi Tanzania ambao watakuwa nyumbani katika Dimba la Ushirika Mkoani Kilimanjaro wakiwakaribisha Mbeya City, Ken Gold dhidi ya FGA Talents Dimba la Sokoine Jijini Mbeya, Mbeya Kwanza dhidi ya Gren Worriors Dimba la Nag’wanda Sijaona Mkoani Mtwara na Dimba la Samora Mkoani Iringa likiwakutanisha Ruvu Shooting dhidi ya Transit Camp.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement