LIGI YA MPIRA WA KIKAPU MAARUFU KAMA TAIFA CUP KUANZAA LEO
Leo ni siku kubwa kwa wapenzi na wadau wakubwa wa mpira wa kikapu Tanzania kwamaana ile ligi kubwa ya mpira wa kikapu Tanzania maarufu kama taifa cup inaanzaa leo kutimua vumbi makao makuu ya nchi
Ligi hii ya taifa cup itajumuisha takribani timu 36 kwa MAANA ya wanaume timu 20 lakini upande wa pili kwa wanawake ni timu 16
Ligi hii hukutanisha mikoa ambayo imeweza kupata nafasi ya kushiriki kwa upande wa wanaume na wanawake na hukutanisha mastaa wote wa mpira wa kikapu Tanzania kwani wakati huu wale wachezaji bora hua wanarudi kutumikia mikoa yao hivyo huleta ushindani mkubwa Sanaa
MSIMU huu wa mwaka 2024 utafanyika Dodoma mara baada ya mwaka jana kufanyika jijini Tanga lakini msimu huu jiji la Dodoma limepata Baraka ya kuandaa michuano hii mikubwaa