Msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika Mechi za mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza kufanyika kati ya Agosti 16 na 18 mwaka huu wa 2024 na marudiano kati ya Agosti 23 na 25, 2024. 

Ni Al Ahly, Espérance, Mamelodi Sundowns, Atlético Petroleos, na TP Mazembe ndio walioondolewa kwenye droo ya raundi ya kwanza ambapo Klabu kutoka Mataifa yatakaowania kurithi mikoba ya Al Ahly kama mabingwa wa michuano hiyo walipatikana katika droo makao makuu ya CAF Cairo nchini Misri.

Ni mechi 54 zikiwa zimepangwa kuchezwa huku baadhi yake zikielezwa kuwa na mvuto zaidi kwa mashabiki huku mchezo kati ya Arta Solar ya Djibouti na Dekadaha FC ya Somalia ukitarajiwa kuvuta hisia.

Young Africans ya Tanzania itamenyana na Vital'o FC ya Burundi, Azam FC pia ya Tanzania ikiwa imepangwa kuvaana na APR FC Rwanda huku FC Nouadhibou ikilazimika kusimamia mechi ngumu ya ugenini dhidi ya Milo FC ya Guinea.

Mara baada ya kutamatika kwa droo hiyo Mkuu wa kitengo cha habari ndani ya klabu ya Yanga Sc Ally Kamwe amewataka wanachama, mashabiki na wapenzi wa Klabu hiyo kutazama zaidi mechi zilizombele yao.

Kwa upande wake Kocha wa Azam FC Youssoph Dabo pia ameeleza wazi kuwa wanajiandaa vizuri ili kuweza kupata ushindi dhidi ya wapinzani wao.

Mshindi wa pambano kati ya El Merreikh na Gor Mahia FC atamenyana na Al Ahly, ambao ni bingwa.

Espérance ya Tunisia itakutana na mshindi wa pambano kati ya Arta Solar na Dekadaha FC katika raundi inayofuata huku mshindi wa pambano kati ya Swallows na Fer Da Beira atamenyana na Mamelodi Sundowns.

Vile vile, mshindi wa mechi kati ya Ngezi Platinium na AS Maniema atachuana na Atlético Petroleos. Timu ya mwisho iliyoondolewa TP Mazembe itamenyana na mshindi wa mechi kati ya Nyasa Big Bullets na Red Arrows.

Raundi ya pili ya hatua za awali za Ligi ya Mabingwa imepangwa kuchezwa Septemba 13-15 kwa mechi za mkondo wa kwanza na Septemba 20-22 kwa marudiano.

Kwa Upande wa Kombe la Shirikisho Afrika, Vigogo Simba SC wataanza katika Raundi ya Kwanza ya wakimenyana na mshindi kati ya Uhamiaji ya Zanzibar na bingwa wa Kombe la FA ya Libya zitakazomenyana katika Raundi ya Awali.

Nayo Coastal Union ya Tanga itaanza ugenini dhidi ya FC Bravos do Maquis ya Angola na ikifanikiwa kuvuka Hatua hiyo itakutana na St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mechi za kwanza za Raundi ya Awali zitapigwa kati ya Agosti 16 na 18, kabla ya timu hizo kurudiana kati ya Agosti 23 na 25.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement