Baada ya kucheza mechi tano bila ushindi, Mashujaa imekiri kupitia kipindi kigumu, huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Adam Adam akisema wanaamini upepo utatulia na burudani itarejea kwa mashabiki,

Timu hiyo ya Kigoma inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza na ilikuwa na mwanzo mzuri ilipocheza mechi tatu bila kupoteza ikishinda mbili na sare moja.

Kwa sasa mambo yameonekana kuwa magumu kwa kucheza dakika 450 bila ushindi na kujikuta nafasi ya 10 ikiwa na pointi nane baada ya michezo tisa.

Maafande hao wanatarajia kushuka tena uwanjani Desemba 2 watakapoikabili KMC katika mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ukiwa wa raundi ya 10 kwa timu hizo,

matokeo siyo mazuri akiahidi kuwa mapumziko ya sasa watayatumia vyema kusahihisha makosa ili kurejesha kasi.

Amesema ligi imekuwa na ushindani mkali kutokana na timu kupata matokeo bila kujali nyumbani au ugenini, lakini bado hawajakata tamaa kubadili upepo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement