Kipa wa Coastal Union, Ley Matampi amechaguliwa mchezaji bora wa mwezi Februari akimshinda kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya (Yanga) na Samson Mbangula (Tanzania Prisons).

Matampi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwa kucheza dakika 270 za mechi tatu bila kuruhusu bao ndani ya mwezi Februari.

Kipa huyo aliiongoza Coastal Union kwenye mchezo dhidi ya KMC ugenini waliotoka suluhu, wakashinda bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji nyumbani na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Pia kamati ya tuzo imemchagua meneja wa Uwanja wa Azam Complex, Amir Juma kuwa meneja bora wa uwanja wa mwezi Februari.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement