LEWIS HAMILTON ANAMPANGO WA KUKIMBIZA MBIO ZA MAGARI FORMULA 1 HADI ATAKOPO KUWA NA UMRI WA MIAKA 40
Lewis Hamilton anasema ataungana na mpinzani wake wa zamani Fernando Alonso katika mbio za Formula 1 "hadi miaka ya 40".
Mkataba mpya wa Alonso wa Aston Martin utamweka kwenye F1 hadi angalau 2026, baada ya kutimiza miaka 45.
Hamilton atakuwa na umri wa miaka 40 mwaka ujao atakapoanza kazi yake na Ferrari, ambayo ni ni makubaliano ya miaka miwili.
"Mimi sio dereva mzee zaidi hapa. Nitaendesha magari kwa muda mrefu sana kwa hivyo ni vizuri Alonso bado yuko," Hamilton alisema.
"Fernando ni mmoja wa madereva bora ambao tumekuwa nao katika mchezo huo kwa hivyo kwa yeye kuendelea kuwa hapa na kuendelea kuwa na matokeo ambayo alikuwa nayo inaonyesha kile kinachowezekana."
Dereva wa McLaren, Lando Norris alisema mafanikio ya Alonso katika kushindana kwa muda mrefu katika kiwango cha juu katika Formula 1 huenda yasionekane tena.
"Yeye ni mmoja wa vijana wa zamani zaidi kushindana juu katika mchezo wowote.” alisema Norris.
Norris, ambaye ako na timu ya McLaren, alisema "anaheshimu sana" uwezo wa Alonso kuendelea kufanya kiwango cha juu kwa muda mrefu.
Kujitolea kwa Alonso na muda mrefu katika F1 kunaweka kiwango kipya - atakuwa dereva wa kwanza kukimbia katika kiwango cha juu hadi miaka ya 40 tangu bingwa wa dunia mara tatu Jack Brabham, ambaye alipata ushindi wake wa mwisho akiwa na umri wa miaka 44 mnamo 1970.
Bingwa mara mbili Graham Hill aliendelea katika F1 hadi alipokuwa na umri wa miaka 46 mnamo 1975, ingawa tofauti na Alonso alitajwa kuwa aliyepita kiwango chake bora katika hatua za mwisho za taaluma yake.