LEBRON JAMES AVUNJA REKODI NBA KWA KUFIKISHA POINTI 40,000
Nyota wa Mpira wa Kikapu, LeBron James amevunja rekodi yake mwenyewe kwa kuwa Mchezaji wa kwanza wa Mchezo huo kufikisha Pointi 40,000 katika historia ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA)
Mwaka 2023, 'King James' anayeichezea Los Angeles Lakers alimpita nyota mkongwe Kareem Abdul-Jabbar aliyekuwa akishikilia rekodi ya Mfungaji Bora wa Muda Wote, na sasa amevunja rekodi yake mwenyewe baada ya ushindi dhidi ya Denver Nuggets
Kwa Pointi hizo, LeBron anakuwa Mchezaji pekee duniani aliyevunja Rekodi za Mastaa Waliofariki (Kobe Bryant Pointi 33,643) Waliostaafu (Kareem Jabar Pointi 38,387, Karl Malone Point 36,928, Michael Jordan Pointi 32,292) na Wanaoendelea Kucheza (Kevin Durant Pointi 28,372)