KYLIAN MBAPPE LEO KUTAMBULISHWA KAMA MCHEZAJI WA MADRID KATIKA DIMBA LA SANTIAGO BERNABEU
Leo ni siku ya utambulisho wa Kylian Mbappe katika dimba la BERNABEU pale Madrid baada ya kusajiliwa kama mchezaji huru kutokea katika Klabu ya PSG ya pale Ufaransa
Stori kubwa ni baada ya kutangaza kua MBAPPE atatambulishwa BERNABEU basi bei za tiketi zote ziliisha muda mfupi na KUWEKA REKODI mpya ya kumaliza ticket zote za watazamaji 85000
Bei ya tiketi imeanzia euro 30 hadi euro 200 ambapo ni sawa na 578147/=Tsh kwajili tu yakuona utambulisho wa MBAPPE siku ya leo
Lakini leo MBAPPE atapewa jezi namba 9 mgongoni ambayo atakwenda kuitumia licha ya kwamba Mbappe anapenda jezi namba 7 na 10 hivyo ataanza jezi namba 9 huenda baadae Modrick akiondoka basi atapewa jezi namba 10
Kubwa lingine ni Mbappe kuvunja REKODI ya Cr7 kwani wakati Cr7 anatambulishwa kulikua na watazamaji 50000 lakini Mbappe ameenda Mbali Zaidi na mashabiki 85000 na tiketi zikaisha mapema kabisaa