mshambuliaji wa Simba aliyekuwa majeruhi, Aubin Kramo amerejea nchini akitokea Ivory Coast na fasta akapanda boti kwenda kuongeza mzuka kikosini mjini Unguja, Zanzibar.

Kramo aliyekuwa Ivory Coast alikoenda kufanyiwa upasuaji wa goti, alitua jana alfajiri na jioni yake alienda Zanzibar, huku akiweka bayana yupo fiti na kilichobaki ni kupiga kazi baada ya kushindwa kuitumikia timu hiyo tangu asajiliwe kutoka Asec Mimosas. Hata hivyo, daktari wa Simba, Edwin Kagabo alisema anasubiri kumuona nyota huyo kabla ya kutoa taarifa rasmi.

baada ya kurejea, Kramo alisema kilichobaki ni mazoezi madogo kutoka kwa daktari ili kumfanya awe fiti zaidi na atakapoona hali yake imeimarika atarudi uwanjani.

Alisema ameimarika kiafya licha ya uwepo wa maumivu madogo na uzito kuongezeka kutokana na kutofanya mazoezi muda mnrefu kwa sababu ya matibabu.

"Niko sawa ninachosubiri ni ratiba ya daktari wa timu ili kuendelea na mazoezi ya viungo na mepesi, halafu tutajua baada ya Ligi kurejea kama nitakuwa sawa,' alisema.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement