KOCHA WA YANGA MIGUEL GAMONDI ATOZWA FAINI YA SH. MILIONI 2 KWA KUWASHAMBULIA WAAMUZI
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtoza Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi faini ya Sh2 milioni kwa kosa la kufanya vurugu ikiwemo kuwashambulia kwa maneno makali waamuzi wa mchezo wa timu yake dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa dakika za jioni na kiungo mshambuliaji Mudathir Yahya.
Gamondi alionekana kutopendezwa na uamuzi wa mwamuzi msaidizi namba mbili, Shaban Mussa baada ya kukataa bao halali la mshambuliaji wa klabu hiyo, Joseph Guede kwa tafsiri yake kuwa alikuwa ameotea.