Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann amelaani utafiti wa hivi majuzi wa "ubaguzi wa rangi" ambao uliwauliza washiriki ikiwa wanataka kuona wachezaji wengi weupe kwenye timu ya taifa ya kandanda.

Kura ya maoni ya shirika la utangazaji la ARD ilisema 21% ya waliohojiwa walikubaliana na pendekezo hilo.

"Ni ubaguzi wa rangi. Ninahisi tunahitaji kuamka. Watu wengi barani Ulaya walilazimika kukimbia.. kutafuta nchi salama," Nagelsmann alisema Jumapili.

Licha huyo mwenye umri wa miaka 36 alisema alikubaliana na kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, ambaye alielezea utafiti huo kama "ubaguzi wa rangi" siku moja kabla.

"Josh [Kimmich] alijibu vizuri sana, kwa maelezo ya wazi na ya kufikiria," Nagelsmann alisema katika mkutano mfupi kwenye uwanja wa mazoezi wa timu yake.

"Nakubaliana naye kabisa. Swali hili ni la kichaa. "Kuna watu huko Uropa ambao wamelazimika kukimbia kwa sababu ya vita, sababu za kiuchumi, majanga ya mazingira, watu ambao wanataka tu kuchukuliwa

"Tunapaswa kuuliza tunafanya nini kwa sasa? Sisi nchini Ujerumani tunafanya vizuri sana, na tunaposema kitu kama hicho, nadhani ni wazimu jinsi tunavyofumbia macho na kuzuia mambo kama hayo."

ARD - shirika la utangazaji la Ujerumani - lilisema limeagiza utafiti huo kuwa na data zinazoweza kupimika, baada ya mwandishi wa habari anayefanya kazi kwenye filamu ya kandanda kuulizwa mara kwa mara kuhusu muundo wa timu ya taifa.

Utafiti huo ulijumuisha washiriki 1,304 waliochaguliwa bila mpangilio.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement