KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya watagomea mualiko wa kushiriki michuano mipya ya Kombe la Dunia la Vilabu ambalo inayotarajiwa kupigwa mwaka 2025.

"Wachezaji na vilabu hawatashiriki katika michuano hiyo. Mchezo mmoja wa Madrid una thamani ya Euro milioni 20 (dola milioni 21.5) huku FIFA ikitaka kutupa kiasi hicho kwa michuano yote. Kama sisi, vilabu vingine pia vitakataa mwaliko huo" Ancelotti 

Badala ya kufanyika mwishoni mwa mwaka, katika mfumo wa mashindano madogo ambayo kwa kawaida huhusisha kucheza nusu fainali na fainali kwa timu itakayoshinda Ligi ya Mabingwa kwenye Kanda tofauti, Kombe la Dunia la Klabu sasa litakuwa likishindaniwa kwa takriban mwezi mzima nchini Marekani mwishoni mwa msimu wa vilabu.

Chanzo kimoja ndani ya Real Madrid kimesema FIFA itawaua wachezaji kwa uchovu huku kikibainisha kuwa kwa kushiriki michuano hiyo wachezaji watalazimika kucheza mechi 72 kwa mwaka 2024/25 kwenye michuano yote.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement