Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 17:60 ya Ligi ya Championship kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kocha wa klabu ya Polisi Tanzania, John Tamba amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) baada yakuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo huo.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 45:2(2.11) ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Klabu ya Polisi Tanzania imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwakosa la kocha wake John Tamba ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo huo, kuonekana katika chumba cha kuvalia wakati wa mapumziko akiendelea na kazi ya kutoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni ya 47:5 ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement