KOCHA WA MANCHESTER CITY PEP GUARDIOLA HUWENDA AKASALIA KLABUNI HAPO KWA MSIMU MMOJA ZAIDI
Mara baada ya kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza kwa misimu minne mfululizo, Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema upo uwezekano wa kuondoka Klabuni hapo.
Guardiola amesema kuwa ukweli ni kwamba anakaribia kuondoka kuliko kubaki huku akiweka wazi kuwa wamezungumza na Klabu na atasaliakwa msimu ujao na wakati wa msimu watazungumza hukuwakitazamia zaidi katika miaka ijayo.
Katika mkutano na wanahabari, Guardiola hakufafanua zaidi ya kusema kwamba alikuwa amechoka kiasili baada ya juhudi nyingine kubwa ambayo iliishia kwa taji la sita katika kipindi cha miaka saba kwa City.
Kocha huyo Raia wa Hispania aliwahakikishia mashabiki kwamba yuko tayari kwa changamoto ya fainali ya Kombe la FA wikendi ijayo dhidi ya Manchester United na bila shaka atapata motisha tena kwa msimu ujao wa Ligi Kuu kama amefanya mara kwa mara.
Guardiola alikuwa mnyenyekevu kuhusu mafanikio yake ya hivi punde, akisema mameneja wengine kama vile Alex Ferguson wa Manchester United walikuwa na mafanikio zaidi kuliko yeye siku za nyuma.