Kocha wa Liverpool Jürgen Klopp ameomba radhi kwa kushindwa kwa Timu yake kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Everton katika kipindi cha miaka 14 na alikiri kwamba hata mbio za Ubingwa ni dhahiri zinafifia.


Klopp ameeleza kuwa wamepambana lakini halikuwa bahati yao na kupoteza kwa bao 2-0 jambo ambalo limemsikitisha kwani hawajawahi kupoteza hapo awali.

Klopp ameeleza kuwa Kwa Sasa wanatakiwa kujioanga kwaajili ya mchezo ujao dhidi ya West Ham.

Klopp ameongeza kwa sasa hawezi kusema kwamba bado wako katika Mbio za Ubingwa Moja kwa Moja kutokana na matokeo hayo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement