Kocha wa Bayern Munich Thomas Tuchel amesema amefarijika baada ya timu yake kuifunga Arsenal 1-0 Jumatano na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Tuchel, ambaye alikua mkufunzi wa kwanza wa Ujerumani kuziongoza timu tatu tofauti kutinga nne bora za Ligi ya Mabingwa, ataondoka Klabuni hapo baada ya msimu kutamatika.

Bayern hawatashinda taji lolote la ndani msimu huu baada ya utawala wao wa miaka 11 kama mabingwa wa Bundesliga kumalizwa na Bayer Leverkusen na matokeo yao mabaya yalisababisha wakubwa wa klabu kuachana na Tuchel mwishoni mwa msimu.


Kwa upande wa Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa hakuna majuto kwa kilichotokea baada ya jitihada za kikosi chake kupambana kumalizika kwa kupoteza kwa mikwaju ya penalti mbele ya Real Madrid.

Guardiola amesema wazi kuwa lengo lake lilikuwa kufuzu hatua inayofuata lakini haikuwa bahati ambapo ametoa pongezi kwa Real Madrid.

Kupoteza kwa City pia kumehitimisha matumaini yao ya kushinda Kombe hilo mara tatu mfululizo na lazima wanajiandaa kwaajili ya mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA Jumamosi dhidi ya Chelsea kwenye Uwanja wa Wembley.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement