Kocha Wa Klabu ya Azam Youssouph Dabo ameeleza ameweka Imani juu ya kikosi chake kufanya makubwa katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kutokana na muda mzuri walionao kwaajili ya maandalizi.

Kocha Dabo ameeleza kuwa kufuzu kushiriki kwa michuano hiyo mara baada ya kushika nafasi ya pili kwenye Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara ni jambo la kwanza lakini kikubwa ni kuhakikisha wanapambana ili kuendeleza mazuri waliyoyafanya.

“Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni magumu na yenye ushindani sana, nlipokuwa na timu Senegal nilishashiriki mashindano haya lakini kwa hii timu niliyonayo na wachezaji tunapaswa kuongeza ubora wa timu na nafikiri kama unamaandalizi mazuri kwaajili ya msimu ujao, Azam FC wanaweza kufuzu hatua ya maiundi n ahata kufanya vizuri lakini tunamuda mzuri na tunataka kumaliza kwanza msimu huu na mechi inayofuata dhidi ya Yanga SC ndipo tutajadili na viongozi kuhusu mambo yaliyombele yetu, ” Amesema Kocha wa Azam FC – Youssouph Dabo.

Kocha Dabo ameeleza kuwa ni takribani miaka tisa Azam FC haijashiiki michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na kueleza kuwa mashindano hayo ni makubwa na magumu na kueleza kuwa kikubwa zaidi ni maandalizi mazuri.

Kwa upande mwingine Kocha Dabo ameelezea juu ya msimu wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara 2023/24 ulivyokuwa kwa upande wao na kuweka wazi kuwa wanafuraha na matokeo na sasa wanahitaji kuiboresa timu ili iweze kukua zaidi.

“Kila mchezo ulikuwa mgumu kwetu na kila mchezo ulikuwa funzo na sasa tunatakiwa kuendelea kukua na kuwa na mabadiliko kwenye timu, na nimewaambia wachezaji wangu wakiwa na mimi au hata nisipokuwepo hii timu inatakiwa kuendelea kukua na kutoa changamoto kwa timu kama Simba na Yanga, ” Amesema Kocha wa Azam FC – Youssouph Dabo.

amezungumza na kuweka wazi kuwa wanajua michuano hiyo ni migumu na licha ya timu hiyo kutokushiriki kwa miaka mingi anakiona kikosi chake kikiwa katika ubora zaidi kwenye mashindano hayo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement