Leo ndio siku ambayo ligi ya Morocco maarufu Kama BOTOLA pro inakwenda kutamatika, Sasa leo TIMU ya kocha NABII Far RABAT watakua nyumbani lakini pia timu ya RAJA CASABLANCA watakua ugenini

Raja Casablanca watacheza ugenini dhidi ya MCO oudja ambao hawa wapo nafasi ya 14 na points zao 25 Lakini Far RABAT watakua na Derby dhidi ya FUS RABAT pale pale jiji la RABAT 

Matumaini ya FAR RABAT yapo kwa timu hii ya MCO oudja kwani ikiifunga timu ya RAJA CASABLANCA au kutoa sare na timu ya FAR RABAT ikishinda basi ATAKUA BINGWA 

Kumbuka RAJA CASABLANCA ana alama 69 lakini FAR RABAT ana alama 68 utofauti ni alama moja tu hivyo kocha NABII ana hizo ndoto za kuchukua ubingwa japo inaonekanaa kua ngumu 

Msimu uliopita Far RABAT ndio walikua mabingwa je wataweza kuuchukua ubingwa mfululizo KITU ambacho katika taifa la Morocco ni kigumu sana kutokea katika historia ya Soka

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement