Kocha msaidizi wa Azam Fc, Youssouph Dabo ametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa alilolifanya baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Tabora United uliochezwa kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Baada ya mchezo huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kocha huyo alitoa kauli zilizotafsiriwa na kamati kuwa ni chafu na za kashfa kwa waamuzi waliochezesha mchezo huo.

Adhabu hiyo ni kwa kuzingatia kanuni ya 45: 2(2.9) ya Ligi Kuu kuhusu kanuni za mchezo.

Klabu ya Azam FC pia imetozwa faini ya Sh1 milioni baada ya wachezaji wake kuchelewa kurudi kiwanjani baada ya mapumziko na kuchelewesha kuanza kwa kipindi cha pili kwa dakika saba.

Adhabu hiyo imetolewa kulingana na kifungu cha 45:2(2-9) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Naye, kocha wa viungo wa Azam Fc, Joao Rodrigues amepewa onyo kali na kamati hiyo kwa kosa la kuinuka kwenye benchi na kwenda jirani na vyumba vya kuvalia bila ruhusa ya mwamuzi wa akiba.

Katika mchezo huo timu hizo ziligawana pointi kwa suluhu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement