Kocha wa Klabu ya Azam Youssouph Dabo amempongeza mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki kwa kuibuka mfungaji bora wa Msimu wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara 2024/25.

Kocha Dabo ameeleza kuwa Aziz ni mchezaji mzuri na mkubwa kwani alishamuona kabla ya Ligi ya Tanzania.

“Kabla sijacheza dhidi yake hapa Tanzania nilishamuona akicheza akiwa na Asec na mimi nilikuwa na timu yangu ya Senegal kwenye michuno ya Ligi ya mabingwa na nilishamuona Pacome na hata Yao Kwasi nawajua, ” Amesema Kocha wa Azam FC – Youssouph Dabo.

Dabo amempongeza na kueleza kuwa kwake amestahili kumaliza katika nafasi ya ufungaji bora wa Ligi kwa msimu huu kwani ni nzuri kwake na hata kwa mustakabali wake.

Kwa upande mwingine Kocha Dabo ameelezea kuelekea katika mchezo wao wa Fainali Kombe la FA na kuweka wazi kuwa huu ni mpira na lolote linaweza kutokea.

“Huu ni mpira na unatakiwa kuwa makini, jumapili sio mbali na ikubwa ni kuomba tuwe sawa kwaajili ya safari na kwaajili ya mchezo huo, ” Amesema Kocha wa Azam FC – Youssouph Dabo.

Kocha Dabo ameeleza kuwa kwa upande ake wanapambana ili kuhakikisha wanashinda kombe hilo japo itakuwa sio mara yake ya kwanza kwenye kazi yake ya kufundisha Mpira.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement